Ndege inayomilikiwa na shirika la ndege la Taiwan (TransAsia) imepata ajali na kuangukia kwenye mto Keelung mji wa Taipei na kuua watu zaidi ya 20.
Taarifa zinasema kuwa watu 58 walikuwa ndani ya ndege hiyo huku watu wameokolewa na kukimbizwa hospitalini na wengine wasiozidi 10 wamenasa katika ndege ambapo waokoaji wamelazimika kuikata ndege hio hili kuokoa watu wengine ambao bado wapo ndani.
Ndege hio ilipita karibu na magari na kudondoka mtoni mda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan Taipei kuelekea uwanja wa ndege Kinmen nje ya Taïwan huku chanzo cha ajari kikiwa bado hakijajulikana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni