Alhamisi, 7 Septemba 2017

SABABU ILIYOMFANYA WAZIRI WA RAIS MAGUFULI KUJIUZULU LEO HII HAPA LIVE!

!

Taarifa :Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, George Simbachawene amejiuzulu.
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ametangaza kujiuzulu nafasi yake kutokana na kutajwa kwenye ripoti za uchunguzi wa tanzanite na almasi.



Akiwasilisha ripoti yake kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Bunge iliyoundwa kuchunguza biashara ya madini ya tanzanite, Dotto Biteko, alisema Simbachawene aulizwe ni kwa nini alitoa uhamisho wa hisa za Sky Associate bila kuhusisha wataalamu kwa sababu kamati ilishindwa kuelewa ni kwa nini alifanya hivyo.
“Kwa muktadha huo, ridhaa iliyotolewa Januari 30, mwaka 2015 na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, George Simbachawene, ina dosari za kisheria na ukiukwaji wa kiutendaji na utoaji wa ridhaa hii, unainyima Stamico kipaumbele cha kununua Kampuni ya TML.

“Kwa msingi huo, kamati imebaini dosari zilizofanywa za kubadilisha watoa maamuzi wa Kampuni ya TLM, zilifanyiwa kazi katika ngazi ya Wizara ya Nishati na Madini chini ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Kamishna wa Nishati na Madini na idara za sheria na katika mashauriano hayo, yafuatayo yalibainika.

“Matokeo ya kuuza hisa Tanzanite One South Afrika, unaipa nguvu Kampuni ya Sky Associate katika Kampuni ya TLM na mauziano hayo yasingeweza kukamilika bila ya kupata kibali cha mheshimiwa waziri.

“Wizara ya Nishati na Madini ilitakiwa kabla ya kutoa ridhaa, ifanye upembuzi yakinifu ili kujua mbia anayeondoka kama anadaiwa chochote kabla ya kuruhusu uhamishaji wa wanahisa, lakini pia kuangalia uwezo wa mbia anayekuja na kujiridhisha maamuzi ya wale wanaouza.

“Tarehe 30 Januari, waziri aliamua kutoa ridhaa bila ya kuzingatia ushauri wa mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na katika hilo, kuna barua ya ushauri wa mwanasheria iliyosema uuzwaji wa hisa hizo sio halali kwa sababu mtu huyo hatumfahamu.

“Pili, Kamishna wa Madini alitoa ushauri kwa waziri, kwamba hili jambo lisifanyike kwani utaratibu haujazingatiwa na pia Kamati ya Nishati na Madini ikiwa chini ya Mheshimiwa Ndassa, ilitoa ushauri ikiwataka wafuate utaratibu.

“Jambo linalosikitisha ni kwamba mheshimiwa Waziri Simbachawene aliapishwa tarehe 24 na tarehe 27 akaingia ofisini na tarehe 30, akasaini hati hiyo bila kuzingatia ushauri uliokuwapo.


Jumatano, 6 Septemba 2017

KAMANDA MKUMBO ASIMULIA JINSI WALIVYOONYESHWA MIILI YA WATOTO



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amefunguka na kusema kuwa jeshi hilo linaendelea kumshikilia kijana Samson Peter (18) ambaye anadaiwa kuwateka watoto wanne na kusababisha vifo vya watoto wawili mkoani Arusha.

Kijana huyo ambaye alikamatwa mkoani Geita akiwa na mtoto mwingine ambaye inasemakana alimteka tena, alipobanwa na jeshi la polisi alikiri wazi kuwa aliwateka yeye hao watoto wanne na kusema kuwa wawili aliwatumbukiza kwenye shimo la choo ambalo lilikuwa halijaanza kutumika kabla ya kwenda Geita ambapo mwisho wa siku walipatwa na umauti. 
"Tulipo mbana aliweza kukiri kwamba anahusika na utekaji wa watoto na alisema kuwa tayari ameshawadhulu hivyo tuliongozana naye mpaka Olasiti ambapo aliweza kuonyesha sehemu ambapo alikuwa amewaua hao watoto na kuweza kuwatumbukiza kwenye shimo la maji machafu katika nyumba mbayo ilikuwa imejengwa hivi karibuni na ilikuwa haikaliwi na mtu yoyote"alisema Kamanda Mkumbo 
Aidha Mkumbo anasema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na kusema pindi uchunguzi ukikamilika wataweza kumfikisha kijana huyo katika vyombo vya sheria, hata hivyo kamanda Mkumbo anadai jeshi la polisi linachukua hatua mathubuti kuweza kuwapata watu wote waliohusika katika utekaji huo. 
"Bahati nzuri watoto wawili waliweza kupatikana mapema hivyo tuliendelea na kuwatafuta watoto wengine wawili pamoja na huyo mtu aliyehusika na utekaji wa watoto hao, watoto ambao hawakuweza kupatikana mapema mmoja alikuwa anaitwa Mauren David Ernest (6) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Lucky Vicent na wa pili Ikram Salum (3) ambaye alikuwa ni mtoto mdogo" alisema Mkumbo 

MIAKA 20 TANGU PRINCESS DIANA AZIKWE, DUNIA BADO INAMKUMBUKA


Princess Diana enzi za uhai wake.
Siku ya mazishi ya Princess Diana.
Siku ya mazishi ya Princess Diana.

Mahali alipozikwa.
Jeneza lenye mwili wake.
Septemba 6, 1997 ni siku ambayo haitasahaulika, pale mkwe wa malkia Elizabeth, Princess Diana alipozikwa jijini London. Miaka 20 imepita lakini bado kila inapofika siku hii, Waingereza hukumbuka kifo chake kwa kuzuru kwenye kaburi lake, kuweka maua na kuwasha mishumaa.
Princess Diana ambaye jina lake halisi alikuwa akiitwa Diana Frances Spencer, alikuwa mke wa mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth, Prince Charles na kabla ya kufikwa na umauti, wawili hao waliofunga ndoa iliyoutikisa ulimwengu Julai 29, 1981, walibahatika kupata watoto wawili, William na Harry.
Kifo chake kilisababishwa na ajali mbaya iliyotokea jijini Paris, Ufaransa kwenye daraja la chini la Pont de l’Alma ambapo mwanamama huyo na watu aliokuwa nao ndani ya gari, akiwemo Dodi Fayed na dereva wao, Henri Paul walipoteza maisha huku mtu mmoja tu, Trevor Rees-Jones akinusurika kwenye ajali hiyo.
Mazishi yake, yalirushwa na kituo cha runinga cha nchini humo na kutazamwa na zaidi ya watu milioni 32.1 nchini humo, achilia mbali mamilioni ya watu kutoka sehemu nyingine duniani waliokuwa wakifuatilia mazishi yake, na kuvunja rekodi kwa kuwa tukio lililotazamwa zaidi kwenye runinga kwa kipindi hicho


RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, AAGANA NA BALOZI WA CHINA AONANA NA MZEE BUTIKU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO



  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva  alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa  Mwakilishi Mkazi wa FAO  nchini Bw.  Fred Kafeero    na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Meshack Malo Ofisa aliyeongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu na kadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw.  Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago  Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing    alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing    alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017


ACACIA YAANZA KUKABIDHI MGODI WA BUZWAGI KWA SERIKALI


Viongozi wa Barick na Acacia wakizungumza na Rais Magufuli, Ikulu. (Picha na maktaba).



BAADA ya Acacia kutangaza kupunguza operesheni zake Bulyanhulu, kampuni hiyo imeanza kuikabidhi Serikali baadhi ya mali zake kwenye Mgodi wa Buzwagi ambao unatarajiwa kufungwa miaka mitatu ijayo.

Katika utekelezaji wa makabidhiano hayo, jana kampuni hiyo iliikabidhi Serikali uwanja wa ndege uliopo katika mgodi huo. Huu ni mgodi wa pili kufungwa na kampuni hiyo baada ya ule wa Tulawaka ambao iliuuza kwa Shirika la Taifa la Madini (Stamico) mwaka 2013.
Jana, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Zainab Telack alisema hiyo ni hatua ya awali katika mchakato wa mgodi huo kusitisha shughuli zake za uchimbaji madini kwa mujibu wa mkataba uliopo.
“Tumeanza na uwanja wa ndege baadaye tutakabidhiwa majengo na vitu vingine kama ulivyo utaratibu,” alisema Telack.
Alisema Desemba mwaka huu utakuwa mwisho wa shughuli za uchimbaji na baada ya hapo wataanza kusaga mawe yaliyochimbwa kwa miaka mitatu mfululizo mpaka 2020.
Juzi, kampuni hiyo ilitoa taarifa ikibainisha lengo lake la kupunguza operesheni zake kwenye Mgodi wa Bulyanhulu baada ya kuzuiwa kusafirisha mchanga wa dhahabu tangu Machi hivyo gharama za uendeshaji kuwa juu kuliko ilivyotarajia huku mapato yakishuka.
Kwa miezi sita ya kutosafirisha mchanga huo, Acacia imedai kuwa imepoteza zaidi ya Sh583 bilioni.
Katika utekelezaji wa mkakati wake wa kubana matumizi, kampuni hiyo inatarajia kupunguza wafanyakazi na kandarasi mbalimbali ilizonazo. Kwa sasa, ina wafanyakazi 1,200 na wakandarasi 800 kwenye Mgodi wa Bulyanhulu.
Taarifa hiyo pia ilibainisha kucheleweshwa kwa leseni za wakandarasi wa machimbo ya chini ya ardhi kwenye Mgodi wa Buzwagi jambo linaloongeza changamoto.
Ingawa mazungumzo baina ya Serikali na kampuni ya Barrick inayomiliki asilimia 64 ya hisa za Acacia bado yanaendelea, uamuzi wa kupunguza operesheni kwenye mgodi huo unatarajiwa kupunguza uzalishaji kwa karati 100,000 kutoka kati ya karati 850,000 hadi 900,000 zilizokadiriwa awali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu, bei ya hisa zake kwenye Soko la London (LSE) ilishuka kwa asilimia sita mpaka Pauni 1.94 huku kwenye Soko la Dar es Salaam (DSE) ikishuka kutoka Sh5,940 mpaka Sh5,400 jana mchana. Tangu kutolewa kwa zuio hilo

KIMBUNGA CHA IRMA CHAFANYIWA MAANDALIZI VISIWANI




Watu wafanya maandalizi ya kujikinga na kimbunga Irma chenye kiwango cha tano na kasi ya nguvu ya upepo hadi kilomita 295 kwa saa, Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga visiwa vya Leeward na kuelekea Puerto Rico, Haiti na Floirda.
Visiwa vingine vilivyomo eneo la eneo la Caribbean vimefanya matayarisho ya mwisho ya kujikinga na kimbunga hicho, Na maafisa wakitoa tahadhari kuwa kimbunga hicho kinaweza kuwa chenye madhara.


MAPUTO KWENYE TUMBO LA SETH , SIRI NZITO YAFICHUKA



Harbinder Singh Seth.

BAADA ya Wakili Joseph Makandege anayemtetea mtuhumiwa wa uhujumu uchumi, Harbinder Singh Seth kuiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mteja wake huyo yupo hatarini kufa kutokana na maputo aliyowekewa tumboni, siri nzito imefichuka, UWAZI linakupasha.

Wakili Makandege alidai mahakamani hapo wiki iliyopita kuwa mahakama ilitoa amri mara mbili ili mteja wake apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili akatibiwe lakini magereza hawajatekeleza amri hiyo. Gazeti hili lilimtafuta Dk. Godfrey Chale ambaye amewahi kuhudumu katika hospitali mbalimbali jijini ikiwemo ya Muhimbili na Temeke na kumuuliza maswali kadhaa kuhusiana na tatizo linalosababisha mtu kuwekewa maputo tumboni, faida yake na athari zake, na kwa nini yanawekwa?
Akitoboa siri hiyo Dk Chale alisema maputo hayo yanawekwa tumboni kama tiba na yanaweza kukaa humo kwa muda mrefu, akafafanua kuwa maputo hayo yaitwayo kitaalamu intra-gastric balloon, ni laini sana na yanaweza kupasuka kirahisi kama mgonjwa hatafuatilia utaratibu wa uchunguzi wa mara kwa mara kuona kama bado yapo sawa na yametengenezwa kwa kutumia madini ya Silicon.
“Maputo huwekwa ndani ya tumbo la chakula na ndani yake huwekwa maji safi ya chumvi yaitwayo sterile salt au saline solution. Puto linapowekwa tumboni, hujaza nusu ya tumbo na muda wote aliyewekewa huhisi tumbo lake limejaa.
Kazi ya maputo haya husaidia kudhibiti hamu ya kula na kujikuta unakula kiasi kidogo sana cha chakula hivyo inakusaidia kudhibiti tatizo la kuongezeka unene kwa kasi,” alisema. Ili kupata undani wa maputo yanayowekwa tumboni, fuatana nasi katika maswali na majibu na Dk. Chale:

KWA NINI MTU ANAWEKEWA PUTO TUMBONI?

“Tiba ya kuwekewa puto inasaidia sana kudhibiti unene, ni njia ambayo siyo ya upasuaji, inapotumika pia husaidia kumuepusha mhusika kupata matatizo ya ini na figo. “Sababu za kuwekewa puto tumboni ni endapo mtu yupo katika hatari ya kupata magonjwa makubwa yanayohusiana na unene ambapo kitaalamu tunasema body mass index (BMI) yake inazidi 35 ambapo inaweza kumsababishia apate kisukari, ini kujaa mafuta, kupanda kwa shinikizo la damu, matatizo ya miguu na kwa mwanamke anapata vivimbe katika vifuko vya mayai au polycystic ovary syndrome.
“Mtu mwenye BMI zaidi ya 35 huwa ni mfupi na mnene sana. Mtu anaweza kuwekewa puto endapo tiba nyingine za kupunguza uzito au unene zimeshindikana, iwe kudhibiti ulaji au matumizi ya dawa za kupunguza unene kushindikana, na hawako tayari kupunguza unene kwa njia ya upasuaji.

PUTO LINAFANYAJE KAZI TUMBONI?

“Puto linapunguza nafasi tumboni hivyo inakusaidia ukila kidogo unahisi umeshiba. Mtu aliyewekewa puto anatakiwa ale chakula maalumu chenye kiwango kidogo cha nishati, awe mara kwa mara karibu na daktari wake, wauguzi na wataalamu wa lishe ili
kuhakikisha puto hilo linaendelea kuwepo bila tatizo.


NINI ATHARI YA KUWA NA PUTO TUMBONI?

“Mara nyingi watu wote waliowekewa puto huwa hawapati athari zozote na wanaendelea na maisha yao kama kawaida ila ni muhumu kuwa karibu na daktari wako kwa mawasiliano na endapo utahisi tatizo lolote basi toa taarifa kwa daktari wako, muuguzi wako au mtaalamu wa lishe.
“Hata hivyo, matatizo yanaweza kutokea mara chache sana inaweza kuumiza njia ya chakula kuanzia kinywani hasa wakati wa kuupitisha lakini ni jambo linalotibika wakati huohuo. Siku za mwanzo baada ya kuwekewa puto tumboni unaweza kujihisi vibaya tumboni, kichefuchefu na kutapika lakini haiendelei kwa muda mrefu.
“Kwa kuwa ni kitu kigeni tumboni, mwanzoni utahisi tumbo linakuwa zito, unacheua asidi mara kwa mara, maumivu ya mgongo na tumbo kujaa gesi lakini baadaye hali hiyo inapotea.

JE PUTO LIKIPASUKA TUMBONI INAKUWAJE?

“Athari mbaya inayoweza kutokea ni endapo puto hilo litanywea lote au kupasuka tumboni kwani husababisha puto hilo liende mbele na kuziba utumbo na tiba yake ni upasuaji wa dharura wa tumbo.
“Kama katika ufanyaji uchunguzi wa mara kwa mara itaonekana puto linaanza kunywea, au tunasema kitaalamu defleted, inamaanisha yale maji ya chumvi yanapungua taratibu, basi puto hilo itabidi litolewe kama lilivyowekwa.
“Kama umewekewa puto, basi hauruhusiwi kusafiri mbali na sehemu walipo wataalamu wako waliokuwekea na endapo itakulazimu usafiri, basi ni vizuri daktari wako akuruhusu na likitokea tatizo wasiliana naye mara moja ili afanye mawasiliano na daktari wa mahali ulipo.

JE PUTO LINAWEZA KUKAA TUMBONI KWA MUDA GANI?

“Muda wa puto kukaa tumboni na kuendelea kufanya kazi ni miezi sita hadi mwaka mmoja kutegemea na aina ya puto lililowekwa, maputo mengi hukaa kwa miezi sita halafu yananywea. “Endapo puto ni la miezi sita, basi lifuatiliwe na kutolewa kwa njia inayoitwa kitaalamu endoscopy. Njia ya kuyaweka huitwa Endoscopic Intragastric Balloon Insertion, na huwekwa tumboni puto moja hadi matatu na kama nilivyosema hukaa si chini ya miezi sita tumboni.

KUNA AINA NGAPI ZA MAPUTO HAYO YA TUMBONI?

“Aina za maputo haya ni nyingi kama vile Spatz, Orbera na Bio Enterics Intra-Gastric Balloon. NINI USHAURI WAKO? “Inashauriwa maputo haya yasikae tumboni kwa zaidi ya miezi sita ili kuepusha kunywea na kuleta madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha kama mgonjwa atachelewa tiba.”

YAPO MADAI KUWA KUNA UVIMBE MWINGINE TUMBONI KAMA PUTO, JE NI KWELI?

“Ni kweli tatizo hilo kitaalamu huitwa spasmodic pains, ni aina ya maumivu makali yanayohusisha mishipa ya fahamu na misuli. Maumivu haya yana tabia ya kuja kwa ukali na kupotea , ni maumivu ya kukata, yakitokea sehemu yeyote ya mwili lazima ukae na ushike sehemu hiyo.
“Spasmodic pains hutokea kwenye misuli ya miguu, ini, moyo, bandama, kongosho na tumbo. Ni maumivu yanayowatokea watoto na watu wazima. Zaidi maumivu haya hutokea tumboni sehemu yoyote lakini wengi hutokea upande wa juu wa tumbo na wanawake hutokea upande wa juu na hata upande wa chini kwenye kizazi hasa pale mwanamke anapokuwa kwenye siku zake, mimba kutishia kutoka na wakati mwingine anapokuwa katika kipindi cha upevushaji mayai au ovulation.

NINI TIBA YA TATIZO HILO?


“Tatizo la maumivu haya huchunguzwa hospitali kutegemea na sehemu yanapojitokeza. Pamoja na kutibu chanzo dawa za kutuliza maumivu haya zinaitwa Antispasmodic, pia zipo dawa za kupaka, kunywa na sindano,” alisema Dk Chale. Seth na James Rugemalira wanakabiliwa na mashitaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi nyaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 22,198, 544. 60 na Sh. 309, 461,300, 158.27. Wote wapo rumande Gereza la Segerea

MAMA SAMIA : NAPIGA GOTI MBELE YA MUME WANGU KUONESHA MAPENZI NA HUBA




Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan, amesema pamoja na wadhfa alionao, lakini mbele ya mume wake atapiga goti ili kuonesha mahaba aliyonayo kwake.
Mheshimiwa Samia Suluhu alitoa kauli hiyo jana Septemba 5,2017 wakati akizindua tamasha la 14 la Jinsia mwaka 2017 lilirotaribiwa na TGNP Mtandao 
na Taasisi ya Mafunzo ya Jinsia (GTI) katika Viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam lenye mada kuu isemayo “ Mageuzi ya Mifumo Kandamizi Kwa Usawa wa Kijinsia na Maendeleo Endelevu”.

Alisema wanawake hawako sawa katika nyanja zote za kijamii na wanatakiwa kutunza mila na desturi nzuri, na kuelezea kuwa hapigi goti kwa mume wake kwa sababu ni mdhaifu 'inferior' ila ni kuonyesha mapenzi na huba.Tushirikiane bila kuacha mila na desturi zetu nzuri,tuende na wanaume katika kuleta maendeleo yetu...hatuko sawa katika nyanja zote za kijamii,mimi na umakamu wangu wa rais mbele ya mume wangu nitapiga goti,na sipigi goti kwamba ni Inferior,hapana!,napiga goti kwa sababu ya huba na mapenzi"..Samia Suluhu



Jumanne, 5 Septemba 2017

USHAURI WA KIBA KWA BONGO MOVIE










Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Seduce me' ameamisha mashambulizi yake upande wa bongo movie na kuwaambia hali mbaya waliyokuwa nayo katika kipindi hiki ni kutokana na kutokuwa na umoja baina yao.

Alikiba ameeleza hayo baada ya kuwepo tetesi ya baadhi ya wasanii wa bongo movie kuwa wanashindwa kusaidiana katika kazi zao na kuogopana jambo ambalo linaleta makundi kati yao na kuwafanya kushindwa kuwa kitu kimoja.

"Mimi siku zote nitawapigania bongo movie kwa sababu wakishafanya kazi zao na kuzipeleka sokoni kwa ajili ya kufanya mauzo ndiyo basi tena lakini sisi wanamuziki tunauwezo wa kufanya 'show' ambazo zitatulinda sisi hata kama wananchi wamesikiliza ngoma zetu na kuzi-download bila malipo hatuwezi kupata hasara kwa kuwa tunategemea show ambazo ndiyo zinalipa, kwa hiyo umoja ni kitu cha msingi sana na ndiyo maana wenzetu wa Nigeria wanasaidiana katika mambo yao na siyo kwamba wanaogopana", amesema Alikiba.

Pamoja na hayo, Alikiba aliendelea kwa kusema "Mimi binafsi ningefurahi sana kama wasanii tungekuwa na umoja, sisi ni wamoja siyo lazima mpaka tukutanishwe kwenye janga fulani!", amesisitiza Alikiba.


Kwa upande mwingine, Alikiba aliendelea kuwashauri wasanii wenzake kuendelea kusaidiana kwa kuwa ni jambo zuri ambalo anaamini litaweza kuwatoa sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwa wasanii wote kwa ujumla bila ya kujali aina ya kazi anazozifanya.

JE UNGEKUWA NDIO BABA MWENYE NYUMBA UNGEMFANYA NINI HUYU MWIZI?


Mwizi aliingia kwenye nyumba ya familia moja kwa ajili ya kuiba. Akiwa ndani mara akasikia nyayo za mtu akija, mwizi akaamua kujificha chini ya meza mahali alipoweza kuona sehemu kadhaa pale sebuleni.

Katika kuangalia kwa makini, akamwona mama aliyeingia akipakua chakula na kuweka kwenye hotpot; mara mama yule akachukua kichupa kidogo kwenye sidiria yake na kumimina kilichokuwemo kwenye kichupa kwenye hotpot kisha akaficha tena kile kichupa.

Mara yule Mama akapotelea mahali ambako alihisi ni chumbani maana alisikia sauti ya mwanaume huko ndani ikisema "haya mume wake, chakula tayari twende tukale."

Muda kidogo ukapita, mumewe alikafika sebuleni na kukaa kwenye meza ya chakula. Alikuwa peje yake, akakaa mezani akamwita mkewe nayr aje kula; mara ikasikika sauti kutoka chumbani ikisrma "endelea mume wangu, mimi naoga kwanza."

Yule mwizi akasikitika sana na kumuonea huruma yule baba akiwa na imani kuwa amewekewa sumu kwenye chakula. Ndipo akaamua kujitokeza na kumuomba radhi yule baba kuwa yeye ni mwizi ila ameona amsaidie kabla hajala kile chakula kwa sababu kilikuwa na sumu. 

Awali yule baba alishtuka akiwa na mchanganyiko wa hasira dhidi ya yule mwizi lakini akajisemea moyoni kwamba ngoja nimfunge kamba kisha hiki chakula nimpe mbwa. 

Yule mwizi akasema "nifanye unachotaka lakini naomba sana usile hicho chakula." Baba akaamua kujaribu kile chakula kama kweli kina sumu kwa kumpa mbwa wao; akamtaka yule mwizi arudi alipokuwa amejifika kisha akamwita mwanawe akampe kile chakula mbwa wao na ahakikishe anakula chote. 

Baada ya kama dakika tano yule mbwa akiwa anaendelea kula kile chakula alianguka na akafa pale pale mwili wake ukiwa umevimba.

JE, UNGEKUWA NDIO BABA MWENYE NYUMBA UNGEMFANYA NINI HUYU MWIZI?

RIPOTI YA MAKINIKIA YA ALMASI NA TANZANITE KUWASILISHWA BUNGENI


Mh Spuka Job Ndungai aikiingia bungeni

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, kesho anatarajiwa kukabidhiwa taarifa za kamati mbili zilizoundwa na Bunge katika Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 kuhusu na makinikia ya almasi na biashara ya madini ya tanzanite.
Kwa mujibu wa taarifa za bunge hafla fupi ya makabidhiano hayo itafanyika katika viwanja vya bunge na viongozi wa kitaifa watakuwepo. Kabla ya Waziri Mkuu kukabidhiwa taarifa hizo, kamati hizo mbili zitakabidhi taarifa zake kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye naye atakabidhi kwa Waziri Mkuu.
Taarifa hizo mbili zinazosubiriwa kwa makini hasa baada ya taarifa za kamati zilizoundwa na Rais John Magufuli kuibua makubwa katika makinikia kwenye makontena bandarini. Kamati hizo maalumu zote zilikuwa na idadi sawa ya wabunge ambao ni tisa na zililenga kushauri juu ya mfumo bora wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa biashara ya madini ya almasi na Tanzanite hapa nchini.
Kamati iliyohusu almasi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ilitajwa kabla ya kuhitimisha shughuli za Bunge la Bajeti. Spika Ndugai aliunda kamati hiyo kupitia Waraka wa Spika namba 3 wa mwaka huu, na kusema: “Kamati hii itatathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya almasi nchini kisha kuandaa mapendekezo mahsusi kwa ajili ya kuishauri Serikali kuhusiana na uendeshaji bora wa biashara ya madini hayo nchini,” alisema.
Uundaji wa kamati hizo umefanyika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kukabiliana na ‘wizi’ wa mali asili za taifa. Wakati akiunda Kamati hizo alisema pia kwamba ilitokana na pendekezo la Rais Magufuli la kuunda Tume ya kuchunguza na kufuatilia madini ya almasi alilolitoa Juni 12 mwaka huu alipohudhuria mkutano wa kupokea Taarifa ya Kamati yake ya Pili ya Kuchunguza Masuala ya Kiuchumi na Kisheria kuhusu usafirishaji wa makinikia, Kamati ya Profesa Nehemia Osoro na pia kutokana na hoja aliyoitoa wakati akikabidhiwa ripoti ya makinikia.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Dk Immaculate Sware Semesi, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Shally Raymond, Mbunge wa Tumbe (CUF), Rashid Ali Abdallah, Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Allan Kiula, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Restituta Mbogo na Mbunge wa Wawi, Ahmed Juma Ngwali (CUF)
Wengine ni Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka (CCM) na Mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Zungu ambaye ni Mwenyekiti. Kamati zote mbili ya almasi na Tanzanite zilitakiwa kuanza kazi Julai 10, na Kituo Kikuu cha kazi kilikuwa katika Ofisi ya Bunge hapa Dodoma.



Aidha, alisema hadidu za rejea za kamati ya almasi ilikuwa ni kuchambua taarifa za Tume na Kamati mbalimbali zilizowahi kuundwa na Serikali kwa ajili ya kushughulikia mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya almasi nchini na kuona Mapendekezo yake na namna yalivyotekelezwa na Serikali.



Nyingine ni Kutathmini mfumo uliopo wa uchimbaji, usimamizi na udhibiti wa biashara ya madini ya almasi nchini na kubainisha manufaa ambayo Serikali inapata kutokana na uwekezaji uliopo katika madini hayo na kubainisha na kushauri kuhusu utaratibu bora unaoweza kutumika katika kusimamia uwekezaji, uchimbaji na biashara ya madini ya almasi nchini.



“Hadidu nyingine ni kushughulikia jambo jingine lolote linalohusiana na mfumo wa uchimbaji, usimamizi na udhibiti wa madini ya almasi nchini,” alisema Kamati ya ufuatiliaji wa uchimbaji wa madini ya Tanzanite yenyewe ilipewa kazi ya kuchakmbua mkataba kati ya shirika la taifa la uchimbaji wa madini Stamico na Tanzania One (TML) na kubainisha faida na hasara kutokana na ubia uliopo. Aidha kamati hiyo pia iliangalia mfumo wa uchimbaji na udhibiti.



(CHANZO: HABARI LEO

SABABU ILIYOMFANYA WAZIRI WA RAIS MAGUFULI KUJIUZULU LEO HII HAPA LIVE!

! Taarifa :Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, George Simbachawene amejiuzulu. Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ametangaza ...