Jumanne, 5 Septemba 2017

JE UNGEKUWA NDIO BABA MWENYE NYUMBA UNGEMFANYA NINI HUYU MWIZI?


Mwizi aliingia kwenye nyumba ya familia moja kwa ajili ya kuiba. Akiwa ndani mara akasikia nyayo za mtu akija, mwizi akaamua kujificha chini ya meza mahali alipoweza kuona sehemu kadhaa pale sebuleni.

Katika kuangalia kwa makini, akamwona mama aliyeingia akipakua chakula na kuweka kwenye hotpot; mara mama yule akachukua kichupa kidogo kwenye sidiria yake na kumimina kilichokuwemo kwenye kichupa kwenye hotpot kisha akaficha tena kile kichupa.

Mara yule Mama akapotelea mahali ambako alihisi ni chumbani maana alisikia sauti ya mwanaume huko ndani ikisema "haya mume wake, chakula tayari twende tukale."

Muda kidogo ukapita, mumewe alikafika sebuleni na kukaa kwenye meza ya chakula. Alikuwa peje yake, akakaa mezani akamwita mkewe nayr aje kula; mara ikasikika sauti kutoka chumbani ikisrma "endelea mume wangu, mimi naoga kwanza."

Yule mwizi akasikitika sana na kumuonea huruma yule baba akiwa na imani kuwa amewekewa sumu kwenye chakula. Ndipo akaamua kujitokeza na kumuomba radhi yule baba kuwa yeye ni mwizi ila ameona amsaidie kabla hajala kile chakula kwa sababu kilikuwa na sumu. 

Awali yule baba alishtuka akiwa na mchanganyiko wa hasira dhidi ya yule mwizi lakini akajisemea moyoni kwamba ngoja nimfunge kamba kisha hiki chakula nimpe mbwa. 

Yule mwizi akasema "nifanye unachotaka lakini naomba sana usile hicho chakula." Baba akaamua kujaribu kile chakula kama kweli kina sumu kwa kumpa mbwa wao; akamtaka yule mwizi arudi alipokuwa amejifika kisha akamwita mwanawe akampe kile chakula mbwa wao na ahakikishe anakula chote. 

Baada ya kama dakika tano yule mbwa akiwa anaendelea kula kile chakula alianguka na akafa pale pale mwili wake ukiwa umevimba.

JE, UNGEKUWA NDIO BABA MWENYE NYUMBA UNGEMFANYA NINI HUYU MWIZI?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SABABU ILIYOMFANYA WAZIRI WA RAIS MAGUFULI KUJIUZULU LEO HII HAPA LIVE!

! Taarifa :Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, George Simbachawene amejiuzulu. Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ametangaza ...