Sanamu ya Askari au Askari Monument ni sanamu iliyopo kwenye kitovu cha jiji la Daressalaam kwenye mahali ambapo mitaa ya Samora na Azikiwe (zamani: Maktaba) zinakutana.
Sanamu inamwonyesha askari Mwafrika katika sare ya kijeshi ya wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914-1918) akishika bunduki yenye kisu cha kando na kutazama upande wa bahari.
Iliwekwa hapa 1927 na Waingereza kama kumbukumbu ya askari na wapagazi Waafrika waliopigania vita hii katika Afrika ya Mashariki hasa kati ya Uingereza na Ujerumani ambao wengi wao walikufa.
Kuna maandishi ya kumbukumbu kwa Kiingereza na Kiswahili kilichondikwa kwa herufi za Kiarabu na herufi za Kilatini pia. Maneno yake kwa Kiswahili ni kama yafuatayo:
"Huu ni ukumbusho wa askari Waafrika wenyeji waliopigana katika Vita Kuu na ni ukumbusho pia kwa wapagazi ambao walikuwa miguu na mikono ya majeshi. Ni ukumbusho pia kwa watu wote waliotumika wakafa kwa ajili ya mfalme na nchi yao katika Afrika ya Mashariki kwenye Vita Kkuu toka mwaka 1914 mpaka 1918 . Ukipigania nchi yako ujapo umekufa watoto wako watalikumbuka jina lako."
Mahali pa sanamu hii iliwahi kuwa na sanamu ya meja Hermann von Wissmann aliyekuwa gavana wa kwanza wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na sanamu hii ilibomolewa na Waingereza walipoteka mji katika mwaka 1916

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni