Jumanne, 5 Septemba 2017

USHAURI WA KIBA KWA BONGO MOVIE










Msanii Alikiba ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake mpya 'Seduce me' ameamisha mashambulizi yake upande wa bongo movie na kuwaambia hali mbaya waliyokuwa nayo katika kipindi hiki ni kutokana na kutokuwa na umoja baina yao.

Alikiba ameeleza hayo baada ya kuwepo tetesi ya baadhi ya wasanii wa bongo movie kuwa wanashindwa kusaidiana katika kazi zao na kuogopana jambo ambalo linaleta makundi kati yao na kuwafanya kushindwa kuwa kitu kimoja.

"Mimi siku zote nitawapigania bongo movie kwa sababu wakishafanya kazi zao na kuzipeleka sokoni kwa ajili ya kufanya mauzo ndiyo basi tena lakini sisi wanamuziki tunauwezo wa kufanya 'show' ambazo zitatulinda sisi hata kama wananchi wamesikiliza ngoma zetu na kuzi-download bila malipo hatuwezi kupata hasara kwa kuwa tunategemea show ambazo ndiyo zinalipa, kwa hiyo umoja ni kitu cha msingi sana na ndiyo maana wenzetu wa Nigeria wanasaidiana katika mambo yao na siyo kwamba wanaogopana", amesema Alikiba.

Pamoja na hayo, Alikiba aliendelea kwa kusema "Mimi binafsi ningefurahi sana kama wasanii tungekuwa na umoja, sisi ni wamoja siyo lazima mpaka tukutanishwe kwenye janga fulani!", amesisitiza Alikiba.


Kwa upande mwingine, Alikiba aliendelea kuwashauri wasanii wenzake kuendelea kusaidiana kwa kuwa ni jambo zuri ambalo anaamini litaweza kuwatoa sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwa wasanii wote kwa ujumla bila ya kujali aina ya kazi anazozifanya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

SABABU ILIYOMFANYA WAZIRI WA RAIS MAGUFULI KUJIUZULU LEO HII HAPA LIVE!

! Taarifa :Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, George Simbachawene amejiuzulu. Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene ametangaza ...